KAIMU SHEIKH WA DAR ES SALAAM AFANYA ZIARA BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA.



KAIMU SHEIKH WA DAR ES SALAAM AFANYA ZIARA BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA.

Mapema leo tulipata neema ya kutembelewa na Sheikh Walid Alhad - Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar Es salaam, aliyefanya ziara rasmi katika chuo chetu cha dini, Hauzat Bilal Temeke na shule yetu ya Bilal Comprehensive zilizopo Temeke, Dar Es Salaam, wiki iliyopita.

Sheikh Walid aliyeambatana na ujumbe wake ulioongozwa na sheikh Zairai Mkoyogole - sheikh wa wilaya ya Temeke amesema, ameitumia ziara hii kujitambulisha kwetu na kufungua mlango wa mashirikiano baina ya ofisi yake na taasisi yetu. 




Comments