MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA TAASISI YA THE DESK AND CHAIR FOUNDATION

 

Mengi wamejionea,wakasema....
"Tulipokuwa tunasoma Shule ya Msingi Nyakahoja ,Mwanza ,Tanzania hatukuwahi kudhani kama tungeondoka na kwenda ughaibuni pasipo kuonana na marafiki zetu na majirani zetu".

Lakini tulipofika kule Ughaibuni tuliendelea na shule na hatukuwahi kuwasahau tuliowaacha Tanzania ,Kupitia Daktari Alhajj Sibtain Meghjee kama Mwenyekiti wa taasisi hii tangu kuanzishwa kwake AGOSTI 2003 hadi leo hii AGOSTI 2023.

katika miaka 20 tumekuwa tukiwafadhili wanafunzi tangu kuanza mpaka kumaliza chuo kikuu na tumekuwa tukiwatibisha wagonjwa na kujenga miundombinu mbalimbali hatukuwahi kuonana ana kwa ana na wale ambao tumewafadhili wala hatukuweza kuona visima vile kwa kuvishika wala majengo yale.....

Tunamshukuru sana Mwenyekiti Alhaj Dokta Captain Muhamad Sibtain ,THE GREATEST OF ALL THE TIME #GOAT amekuwa daraja takatifu kwa dua zetu ,sadaka zetu,funga zetu,ibada zetu na matendo yetu mengi ya kiimani kupokelewa sababu ya uaminifu wake na ubunifu wake uliotukuka."
"Tunawaombea wale wote Mwenyezimungu awabariki

TUNAMSHUKURU SANA MWENYEKITI DR.SIBTAIN KWA UKARIMU ,UNYENYEKEVU,UBUNIFU,UCHAPAKAZI,UPENDO,HURUMA,NA MAJITOLEO MATAKATIFU"
"Inaleta faraja,heshima na inatia moyo sana pale ambapo unaenda kukutana na matabasamu ya watu ambao unaambiwa ile sadaka uliyoitoa ndio imemponyesha huyu na ukikumbuka mgonjwa ulimuona tu kwenye picha hofu ikakujaa lakini sadaka yako imemponyesha"

Nimefarijika kuiona miradi yote iliyofanywa na The Desk And Chair Foundation

Comments