24 Dhulhija ni
EID MUBAHALA
MAANA YA MUBAHALA:
Kilugha:Ni neno la Kiarabu lenye maana ya Kuapizana au Kulaaniana,_
Kisheria: _Kitendo cha watu wawili au pande mbili kila moja ikiamini Imani yake ni sahihi, kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu amlaani aliye katika Imani ya Makosa ili ukweli halisi ujulikane._
CHANZO CHA TUKIO LA MAAPIZANO:
Mtume (saw) aliandika barua kwa Askofu mkuu wa mji wa Najran kumlingania yeye na watu wake wakubali Uislamu.
Wakristo wa Najran wakaamua kutuma ujumbe wa watu zaidi ya 10 kwenda Madina kuongea na Mtume (s) Ujumbe uliongozwa na Viongozi 3 ambao ni ``` *Aqib, Sayyid na Abuu Haritha.* ```Ujumbe huu ulifanya mazungumzo ya kina na Mtume ndani ya msikiti wa Mtume (saw) Madina.
```
MAAZIMIO YA KUFANYA MAAPIZANO (MUBAHALA)
Mwishoni kila upande ulibakia na msimamo wake ukiamini ni sahihi kuliko wa Mwenzake, Wakaamua kikao kifunge kwa Maapizano (Mubahala) Wkaamua kuwa siku inayofuatia iandalie kwa ajili ya Mubahala nje kidogo ya mji wa Madina eneo la jangwani.`
MISIMAMO YA PANDE MBILI:
Upande wa Uislamu (Mtume Muhammad), alisimama juu ya Imani..``` *_"Hakika mfano wa Isa (a.s.) mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, aliumbwa kwa udongo kisha akamwambia: Kuwa naye akawa._* "Quraan (3:59)
Na hivyo Nabii Issa (Yesu) Sio Mungu.```
Upande wa Wakristo wa Najran ukiongozwa na (Abu Haritha):
Kwa kuwa Nabii Isa alizaliwa bila baba, Wakristo wakabakia na Imani yao kuwa baba yake ni Mwenyezi Mungu na hivyo kumfanya ni Mwana wa Mungu._
AMRI YA MUNGU KWA MTUME MUHAMMADI
Ujumbe wa wakristo uipokataa kukubaliana na hoja hii, Mwenyezi Mungu akateremsha Aya:-```
"Na atakayehojiana nawe (Muhammad) katika hili baada ya ujuzi uliokufikia, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafis zenu, kisha tuombe kwa kunyenyekea tuijaalie laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie wenye kusema uongo."_* Quran (3:61)
SIKU YA MAAPIZANO:*
24 DhulHijaa (Mfungo Tatu) Mwaka 10 Hijiria`
UPANDE WA MUHAMMAD ALITOKA NANI:
Baada ya Kushuka Quran (3:61) Asubuhi iliyofuata Mtume akaenda nyimba kwa Imam Ali na kumchukua``` *Imam Hassan* ```kwa mkono wake wa kuume na``` *Imam Hussein* ``kwenye mkono mwingine kisha akamtaka``` *Imam Ali* na *Bi Fatma Zahraa* `waongozane nae.
MATOKEO YA KIKO CHA MAAPIZANO:
`Baada ya Askofu mkuu kuona nyuso za watu waliotoka na Mtume Muhammad alisema kuwaambia wanzake``` *_"Enyi Wakristo: Mimi naziona nyuso hizi (kundi la Mtume) kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, Wallahi atauondoa. Msiapizane naye mtaangamia, na hatabaki Mkristo ye yote hapa duniani mpaka siku ya Kiama."
Alipoulizwa Ahtam, akawaambia: Niacheni nikamuulize Muhammad, alipomkabili Mtume akamuuliza, ``` *_"Ewe Abulqasim unatoka na kina nani kwa ajili ya maapizano?"
```Mtume (s.a.w.) akamjibu:``` *_"Ninaapizana nanyi nikiwa na watu bora hapa duniani na watukufu mno mbele ya Mwenyezi Mungu, nao ni hawa (akawaonyesha) Ali, Fatima, Hasan na Husein."_*
```
Wakaogopa kuapizana na Mtume, na badala yake wakaomba sulhu kwa Mtume (s.a.w.) kwa kutoa dirham arobaini elfu.

♧ *_Tarikh Ibn Athir J.2 Uk. 200_*
♧ *_Tafsirul Qurtubi J.4 Uk. 104_*
♧ *_Tafsirul Ibn Kathir J.1 Uk. 376-379_*
♧ *_Tafsirul Khazin J.1 Uk. 359-360_*
♧ *_Tafsirul Maragh J.3 Uk. 175_*
♧ *_Tafsirul Kabir J.8 Uk. 81_*
♧ *_Zadul Masir J.1 UK. 399_*
Comments
Post a Comment