Naibu Mudir wa Hawza Imam Swadiq na Mjumbe wa bodi ya wazamini T.I.C Samahat Sheikh Mohamed Abdi Mbwana akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada kwa kituo cha afya cha kigogo jijini Dar es salaam, msada huo umeandaliwa na Hawza Imam Swadiq (a.s).
HOSPITALI YA KIGOGO. Waumini wa dini ya kislam nchini wametakiwa kuwa na moyo wa kusaidia watu hususani wenye uhitaji kwani kwa kufanya hiyo ni moja ya mafundisho ambayo alikuwa akifundisha mtume Muhammad (s.a.w.w).
Akizungumza jana 26/07/2023 sawa na Muharramu 8/ 1445 jijini Dar es salaam na Naibu Mudir wa Hawza Imam Swadiq (a.s) na Mjumbe wa bodi ya wadhamini T.I.C, SSheikh Mohamed Abdi Mbwana mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha kigogo na kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo vya kufanyia usafi.
Katika ziada hiyo ambayo sheikh Sheikh Mohamed Abdi Mbwana aliongozana na viongozi mbalimbali akiwepo Afisa Mtendaji wa kigogo ndg Reginald Maina pamoja Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa Ndugu. Rashidi Ally Luwoga.
Alisema kwa kwakutambua mchango mkubwa wa watendaji wa kituo hicho kwa namna ambavyo wamekuwa wakitoa huduma za afya hivyo kama jamiiwameona watoe msaada huo kwa lemgo la kuonyesha wanatambua mchango wao.
"Leo tumekuja kutoa msaada wa vifaa mbambali vya usafi, na vifaa vingine ikiwemo katoni za maji kwa lengo la kuunga mkono mchango wao hasa kwa kutoa huduma jamii" Alisema Sheikh Mbwana.
Alisema jamii hususani waumini wa dini ya kiislam nchini kuwa na moyo wa kujitolea kusaidia hasakwa wale walio na mahitaji kwa kufanya hivyo ni kuenzi mafunzisho na matendo ya mtume Muhammad.
Kwa upande wao Afisa Mtendaji wa kigogo ndg Reginald Maina pamoja Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa Ndugu. Rashidi Ally Luwoga wametoa shukrani kwa msaada huo kwani hutasaidia kuongeza ufanisi hasa katika kutoa huduma za afya.
"Tuchukue nafasi hii kutoa shukrani zetu kwa niaba ya wananchi na wakazi wa kigogo kwa msaada huu kwani utasaidia kuwezesha kituo hiki kuendelea kutoa hudumabora zaidi" Walisema.
Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa Ndugu. Rashidi Ally Luwoga akifafanua jambo mara baada ya kupokea msaada katika kituo cha afya cha kigogo jijini Dar es salaam.
Comments
Post a Comment