Dkt. Mohamed Swalehe Kanju ni Mwislamu wa Madhehebu ya Shia Ithna'ashariyyah, alizaliwa mwaka 1940, ni mwenyeji wa Mkoa wa Tanga, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania-TIC na 1992 yeye alikuwa miongoni mwa washiriki katika Kikao cha kwanza kwenye kuchagua Viongozi wa TIC, kikao hicho kilifanyika katika Hawza Bilal Temeke, Dar es Salaam.
Dkt. Mohamed Kanju alikuwa mstari wa mbele katika kuwatumikia Ahlulbayt (a.s) katika nyanja mbalimbali ikiwemo kutarjuma Vitabu kwa lugha ya Kiswahili kupitia Taasisi ya Bilal Muslim Mission of Tanzania na ufanyaji wa Majilisi katika kijiji cha Mkumbara, Mkoa wa Tanga, ikiwa sambamba na kupinga dhulma duniani ikiwemo ya Palestina katika Masjid al Aqswa.
Yafuatayo ni matukio yameyofanyika leo katika Masjid Ghadir, Makao Makuu ya Jumuiya ya Shia Ithn'ashariyyah Tanzania-TIC Kigogo, Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment