𝗗𝗢𝗡𝗗𝗢𝗢 𝗭𝗔 𝗙𝗘𝗜𝗦𝗔𝗟 𝗣𝗢𝗪𝗘𝗥 𝗕𝗥𝗘𝗔𝗞𝗙𝗔𝗦𝗧 𝗖𝗟𝗢𝗨𝗗𝗦 LEO HII



 -Nilikuja bara na timu yangu ya JKU kwenye mashindano ya kagame cup na ndipo Yanga na Simba waliniona,Ila timu ya kwanza kunitaka walikuwa Simba ambao walinipa ofa ya 25m ila Mimi nilikuwa nataka 60m na Haji manara ndio alinipeleka kwa Viongozi wa Simba Ila tukashindwana.

Niliamua kwenda Yanga kwasababu ya mapenzi yangu tu, kwasababu nilitamani kucheza Yanga licha ya kipato kidogo ambacho walinipa Yanga kipindi kile.
Na Ugali na sukari nilikuwa nakula kipindi cha Uongozi ule uliopita siyo huu wa sasa.
-Unajua Mimi kingereza sijui ndio maana unaona yote aya, Kwasababu mkataba ambao nilisaini ulikuwa umeandikwa kingereza mtupu,na mkataba ulikuwa wa miaka 3 na Mimi nilijua nasaini mkataba wa miaka 2 Kama tulivyokubalina mdomoni,Kwenye mkataba huu tulikubaliana ada ya usajili 100m.Lakini huwezi kuamini sikupewa pesa yote walinipa 10m mwanzoni,,baadae wakaja wakanipa 20m,Nailiobaki ilikuwa mbinde kulipana.
-Rais Eng Hersi Said Mimi ndio naugomvi nae kwasababu ilifika kipindi alikuwa hataki kupokea simu zangu,Nikipokuwa nataka pesa yangu nimaliziwe ilifikia hadi wakati hata simu za mama yangu na baba yang hawakutaka kuwapokelea ndipo nikaongea na mwanasheria wangu kuhusu tatizo hili,Na mwanasheria wangu akasema mkataba ambao nilikuwa nimesaini Yanga waliniambia watanilipa pesa yangu kwa mafungu ndani ya mwaka mmoja.
-Mimi wazazi wangu wote ni Yanga ndio maana hata nilipochagua kucheza Yanga bado mama yangu alinambia nivumilie ipo siku nitakuwa sawa kifedha ndio maana nilisaini kwa dau sana kipindi nakuja Yanga sc.Naomba msaada kwa Watanzania wenzangu ili niende CAS kuipambania haki yangu na hata Kama nitashindwa kesi moyo wangu haupo tayari kurudi Yanga SC.

"Hata Leo akiondoka Hersi ninarudi sasa hivi Yanga SC, pia Ghalib kaniudhi alikua hashiki simu zangu kabla, Amenitafuta baada ya kuondoka na mimi sikupokea kwasababu sipendi dharau hata kama sina kitu"

Comments