Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ametahadharisha kuwa, iwapo utawala haramu wa Kizayuni wa Israel utafanya mahesabu ghalati, basi ujiandae kukabiliwa kwa makombora ya wanamuqawama.
Sayyid Hashim Safiuddin amesema hayo katika mahojiano maalum na shirika la habari la Tasnim na kuongeza kuwa, Katibu Mkuu wa Hizbullah Sayyid Hassan Nasrullah ameonya mara kadhaa kwamba, mahesabu yoyote yasiyo sahihi ya Wazayuni yatajibiwa kwa makombora ya wanamuqawama yatakayolenga Tel Aviv.
Afisa huyo mwandamizi wa Hizbullah ya Lebanon amesema hesabu ghalati za utawala huo pandikizi zitapelekea Hizbullah itume kikosi cha Ridhwan katika mji wa al-Jalil unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo ghasibu.
Safiuddin ameashiria luteka ya kijeshi iliyofanywa hivi karibuni na kikosi hicho maalumu cha Ridhwan, ambacho kinazishughulisha mno na kuzikosesha raha duru za Israel na kusema kuwa, mazoezi hayo yalitoa ujumbe mzito na wa wazi kwamba Hizbullah daima ipo tayari na imejiandaa kwa chochote.
Ameeleza bayana kuwa, Hizbullah iko tayari kwa ajili ya kukabiliana na uwezekano wa kujitokeza mvutano katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa kwa mabavu, na kamwe haitamruhusu adui Mzayuni kuendelea na uchokozi wake.

Mjumbe huyo wa Hizbullah pia amesema harakati hiyo ya muqawama inaendelea kuimarika na kupata nguvu, huku akieleza bayana kwamba wakati wa kusambaratishwa na kutimuliwa Israel katika eneo la Asia Magharibi unazidi kujongea kwa kasi.
Ameongeza kuwa, jamii ya utawala pandikizi wa Israel inaedelea kuporomoka ndani kwa ndani, na haina tena viongozi wa kihistoria, na kwamba watalawa wa hivi sasa wanakabiliwa na tuhuma za ufisadi na rushwa. Sayyid Safiuddin amesema aghalabu ya viongozi hao wa Kizayuni karibuni hivi wataishia jela kwa jinai zao.
Comments
Post a Comment