Vitendo vya hujuma na chuki dhidi ya Uislamu vinaripotiwa kukithiri mno nchini Sweden. Ripoti zinaeleza kuwa, Sweden imekuwa na kuwa kituo cha vitendo vya kikafiri dhidi ya matukufu ya Kiislamu.
Matukio ya kuuchomwa moto nakala za kitabu kitukufu cha Qur'an yamefanyika mara kadhaa hadharani.
Viongozi wa Sweden wameendelea kutoa kauli za kinafiki za kutetea vitendo hivyo wakidai ni uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.
Caroline Kassem, mmoja wa viongozi wa chama cha Nyas amekosia vikali utendaji wa serikali ya Sweden kuhusiana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu.
Mwanasiasa huyo ameashiria kuufungwa baadhi ya shule za Waislamu nchini Uswidi na kueleza kwamba, shule za kidini za Kiislamu ndizo zinazofungwa ilhali shule za dini nyingine hazibughudhiwi wala kuguswa.

Uchunguzi wa maoni uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Sifo huko Sweden umeonyesha kuwa asilimia 51 ya wananchi wa nchi hiyo wanataka kupigwa marufuku vitendo vya kuidhalilisha Qur'ani Tukufu na vitabu vingine vitukufu.
Rasmus Paludan mwanasiasa mwenye misimamo mikali ya kibaguzi ambaye ni mkuu wa chama cha mrengo wa kulia chenye misimamo ya kufurutu ada cha huko Denmark miezi kadhaa iliyopita alichoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu karibu na ubalozi wa Uturuki mjini Stockholm chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Kitendo hicho cha Paludan kililaaniwa vikali na Waislamu na nchi za Kiislamu. Waislamu na nchi za Kiislamu ziliikosoa serikali ya Sweden kwa kushindwa kuzuia hujuma hiyo dhidi ya Waislamu na matukufu yao.
Comments
Post a Comment