Wanaume wawili waliokuwa wametiwa hatiani kwa kukufuru, kuidhalilisha Qur’ani Tukufu, na kuutukana Uislamu, Mtume Muhammad (SAW), na matakatifu mengine ya Kiislamu wamenyongwa nchini Iran.
Kwa mujibu wa kituo cha Hhbari cha Idara ya Mahakama, Mizan, Yousef Mehrdad na Sadrollah Fazeli Zare, waliokuwa wakivunjia heshima matakatifu ya Waislamu wa dunia na maadili ya kitamaduni na kidini ya watu wa Iran, wamekuwa wakiendesha kampeni katika mitandao ya kijamii, wakitukana dini ya Uislamu, Mtume Muhammad (saw) na maimamu wa watoharifu katika kizazi chake na kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu.
Mtandao wa habari wa Idara ya Mahakama ya Iran, Mizan, umesema: Mehrdad alikuwa ameunda kundi la mtandaoni lililokuwa likieneza chuki dhidi ya Uislamu, kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu na kumtukana Mtume Muhammad (SAW) na Ahlubaiti wake watoharifu (as), na alikuwa akitumia akaunti mbili tofauti kwa ajili ya shughuli hizo zilizokuwa na nambari ya rununu ya Irani na nyingine ilikuwa ikitumia nambari ya Ufaransa.
Uchunguzi mpana na wa kina, pamoja na maungamo yake yaliyoandikwa, ulifichua kwamba Mehrdad amekuwa akifanya kazi kubwa sana kuhimiza watu kumkufuru Mwenyezi Mungu na kuvunjia heshima matukufu ya kidini.
Mehrdad alikuwa msimamizi wa vikundi visivyopungua 15 vya mtandaoni vinavyopiga vita Uislamu.
Mhalifu mwenzake, Sadrollah Fazeli Zare, amesimamia vikundi na vituo 20 vya kupinga dini na kuvunjia heshima Uislamu.
Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa na mahakama, Sadrollah Fazeli Zare amepatikana na hatia ya kumtukana Mtume (saw), kuritadi, kumvunjia heshima mama yake Mtume (saw), kuidharau Qur’ani kwa kuichoma moto, na kuchapisha picha za faragha za watu wengine bila ya ridhaa yao; na Yousef Mehrdad, amepatikana na hatia ya kumtusi Mtuume (saw) na kuvunjia heshima matukufu mengine ya kidini na Kiislamu. Wawili hao walinyongwa mapema leo
Comments
Post a Comment