WAKATI klabu ya Yanga ikiwa mchezo wao wa nusu fainali ya kombe la Shirikisho Azam dhidi ya Singida Big Stars kusogezwa mbele, wapinzani wao kwenye nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, Marumo Gallants wanaendelea na mechi zao kama kawaida.
Yanga iliandika barua rasmi ya kuomba mchezo wao wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Azam uliotakiwa kuchezwa Mei 7 usogezwe mbele na TFF tayari imeweka Rasmi kuchezwa tarehe 21 Mei 2023 kwa lengo la kupisha maandalizi kwa ajili ya mechi dhidi ya Marumo.
Marumo Jumatano ya wiki hii ilikuwa na mechi (Ugenini) ya Ligi Kuu dhidi ya Maritzburg na mchezo huo ulimalizika kwa sare 2-2.
Comments
Post a Comment