Sheikh Mkuu wa Waithna'ashariyyah Tanzania aongea mbele ya Wajumbe wa JMAT

Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania Maulana Sheikh Hemedi Jalala akiongea mbele ya Wajumbe wenzake wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania-JMAT  katika mkutano mkuu Maalum wa Jumuiya hiyo, leo 10 Mei, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Ambapo katika mkutano huo amehudhuria Naibu Waziri wa Mambo ya ndani  nchini Mhe. Jumanne Abdallah Sagine akimuwakilisha Mgeni Rasmi Mh. Dkt. Philip Isdori Mpango Makamo wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania lengo kuu la chombo hicho ni kuwaunganisha / kuwakusanya  Watanzania wote bila kujali  Dini na madhehebu yao kwa lengo la kuenzi na kudumisha Amani ya Tanzania.







Comments