"Mambo matano yatakayo tatua changamoto ya kimalezi katika jamii
ni wazazi kuwa makini na kuwaangalia watoto katika malezi, viongozi wa dini kusimama katika kuhamrisha mema na kukataza maovu, Jamii kuwa makini na kukatazana, Serekali kwa upande wa serekali wao wananguvu ya kuzuiya maovu yote yanayoendelea katika jamii na ni kushirikiana kwa watu wote wananchi na viongozi wa pande zote mbili".
Hayo yalisemwa jana (27 Mei, 2023) na Mjumbe wa bodi ya Wadhamini wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania (TIC) na Naibu Mudir wa Hawzat Imam swadiq (a.s) Sheikh Mohammed Abdi katika Kongamano la kupinga Ukatili wa Kijinsia, katika ukumbi wa TIC Makao Makuu, Dar es Salaam.
Katika Kongamano hilo lilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali ikiwemo Jesho la Polisi, Viongozi wa Dini, Wadau wa Jeshi la Polisi katika kupinga Ukatili wa Jinsia na Wananchi wa dini zote.
Comments
Post a Comment