
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina ushirikiano wa kistratejia na
Syria, na hilo limethibitishwa na uungaji mkono wa Tehran kwa serikali
halali ya nchi hiyo wakati wote wa mgogoro wa Syria na kuisaidia
serikali ya rais Bashar al-Assad katika harakati za kupambana na makundi
mbalimbali ya kigaidi.
Baada ya kushindwa kundi la kigaidi la DAESH (ISIS), uhusiano wa
Syria na Iran hivi sasa umepanuka na kujumuisha nyuga mbalimbali, na
kuna matarajio ya wazi ya kustawishwa uhusiano huo katika nyanja zote.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Jamhuri ya Kiislamu ya
Iran IRNA, Dk David N. Yaghoubian, Profesa wa historia katika Chuo Kikuu
cha Jimbo la California, amesema kuhusu ziara ya Rais Ebrahim Raisi
nchini Syria kwamba ziara hiyo imepanua wigo wa umoja wa kihistoria
ambao umekuwa na ulazima kwa nchi hizo mbili katika nyakati za mgogoro
mkubwa na vinapoibuka vitisho dhidi ya mamlaka ya kitaifa ya mataifa
hayo.
Profesa Yaghoubian ameongeza kuwa Marekani haiungi mkono kurejeshwa uhusiano kati ya Syria na nchi zingine kwa sababu hatua hiyo ni kiashiria cha kushindwa rasmi vita vichafu vya Marekani dhidi ya Syria, ambapo mabilioni ya dola yalitumika kusaidia magenge ya kigaidi ya ukufurishaji yaliyokuwa na lengo la kuipindua serikali ya Syria, kuigawanya vipande vipande nchi hiyo na kuuweka madarakani utawala kibaraka utakaounga mkono utawala wa kibaguzi wa Israel na kuafiki kuporwa na utawala huo Miinuko ya Golan ya Syria.
Tarehe 3 Mei, Ayatullah Seyed Ebrahim Raisi, Rais wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran, alitembelea Syria kwa mwaliko rasmi wa Rais Bashar
al-Assad wa nchi hiyo akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa maafisa wa
kisiasa na kiuchumi. Safari hiyo ni ziara ya kwanza ya rais wa Iran
nchini Syria tangu mwaka 2011 ulipoanza mgogoro wa nchi hio.
Katika ziara hiyo, maafisa waandamizi wa Iran na Syria walitia
saini hati 14 za ushirikiano katika nyanja mbalimbali katika hafla
iliyohudhuriwa na marais Raisi na Assad...
Comments
Post a Comment