Benki ya CRDB kupitia kitengo cha Al Barakah leo imezindua mikopo maalum ya Hija na Umrah isiyo na riba ili kuwawezesha mahujaji kutimiza ibada hizo.
Mikopo hiyo ya Hija na Umrah inayotolewa kupitia huduma zinazofuata misingi ya sharia ni suluhisho kwa waumini wa dini ya Kiislam ambao wanataka kufanya safari ya Hija lakini wana changamoto za kifedha.
Kwa kulitambua hilo, Benki ya CRDB inawawezesha kulipia gharama za usafiri na malazi. Uzinduzi wa bidhaa hii mpya umefanyika wakati Waislamu kote duniani wakijiandaa kutekeleza ibada za Hija na Umrah. Mwaka huu, Tanzania ina nafasi ya kupwapeleka hadi mahujaji 3,000 lakini wengi hawana fedha za kutosha kugharimia safari zao.
Mikopo hii inatolewa hadi Shilingi milioni 30. Kwa wateja ambao ni wafanyakazi, Benki inafanya uwezeshaji wa hadi asilimia 80 ya gharama zote za safari na kwa wafanyabiashara inatoa hadi asilimia 50.
Katika hafla ya uzinduzi, Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kufadhili Hija na Umrah na kuwahamasisha Waislam nchini kuitumia fursa hiyo kutimiza ibada hizo muhimu.
Comments
Post a Comment