Mkuu wa vyuo vya kidini nchini Iran amesema: dini zote zinapaswa kusimama imara na kupinga dhulma na ukandamizaji wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Shirika la habari la Mehr limeripoti kuwa, Ayatullah Alireza
Arafi, Mkuu wa vyuo vya kidini nchini Iran amekutana na kufanya
mazungumzo na Mar Awa Royel III Kiongozi mkuu wa Kanisa la Assyrian la
Mashariki, ambapo amesisitiza kwa kusema, kutokana na changamoto
zinazoikabili jamii ya wanadamu hii leo, dini zinapaswa kutoa mchango
chanya na wa ujengaji na akaongeza kuwa: mfumo wa udhibiti na wa
dhulma uliopo katika milingano ya kimataifa haukubaliwi na mtu yeyote na
kuna ulazima kwa dini zote kuchukua hatua zilizoratibiwa kwa pamoja
dhidi ya udhalimu huo.
Ayatullah Arafi amebainisha kuwa: kuporomoka kwa familia ambayo ni
kitovu kikuu cha jamii ni mojawapo ya changamoto ambazo dini zinapaswa
kuchukua hatua ya kuizuia ili kuepusha ongezeko la madhara na uharibifu
wake.

Mkuu wa vyuo vya kidini nchini amesisitiza kuwa: mbali na dini kulinda utambulisho wao, zinapaswa kuelewana na kuchukua hatua za pamoja katika maeneo yanayoziunganisha.
Ayatullah Arafi amesema, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilisimama
imara dhidi ya fikra potovu za kundi la kigaidi na ukufurishaji la DAESH
(ISIS) na leo hii inasimama imara kukabiliana na utawala wa Kizayuni na
akabainisha kwamba: Iran iko bega kwa bega na ndugu zake Waislamu wa
Kisuni huko Palestina na inajitoa mhanga katika njia ya kuwatetea
wapendwa wake hao, hivyo ni wajibu na jukumu la watu wote kusimama imara
na kukabiliana na dhulma za utawala wa Kizayuni wa Israel...
Comments
Post a Comment